RC: Marufuku Kuwasha Moto Nyumbani Bila Kibali Dodoma

 

RC: Marufuku kuwasha moto nyumbani bila kibali Dodoma

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amewataka watendaji wa Mkoa huo hususani wa ngazi za vitongoji na vijiji kumsimamia Sheria ndogondogo walizojiwekea hasa kwa kuwawajibisha watu wanaowasha moto bila kufuata kibali


Senyamule ameyasema hayo Oct 8,2024 kwenye Hafla ya uzinduzi wa kampeni ya usalama dhidi ya moto Mkoa wa Dodoma


Senyamule amesema kuwa anafahamu kuwa Kuna vijiji na Mitaa ambayo wametunga Sheria ya kuwaajibisha watu wanaowasha moto bila kuomba kibali ili kutunza uoto wa asili na kuepuka majanga ya moto


Aidha Senyamule amezikumbusha Taasisi mbalimbali kuweka tahadhari ya majanga ya moto katika majengo yao ili kuepusha majanga ya moto ambayo yanaleta hasara kubwa Kwa Serikali


Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Dodoma Mrakibu. Rehema Menda amesema kuwa kuanzia mwezi January mpaka mwezi Septemba mwaka huu 2024 wamepata miito ya moto 2013 ambayo ilipelekea majeruhi 16 na vifo vya watu 9 lakini pia wamepata wito wa maokozi 86 ambapo maokozi hayo ni ya majini na Barabarani na vifo vya majanga hayo ni vya watu 36

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad