Ripoti ya Uchunguzi Maiti ya Mohbad iko Tayari

 

Ripoti ya Uchunguzi Maiti ya Mohbad iko Tayari

Ripoti ya uchunguzi wa maiti (toxicology) na uchambuzi mwingine wa kitaalamu uliofanywa nchini Marekani kuhusu rapa marehemu, Ilerioluwa Oladimeji Aloba maarufu kama Mohbad umetoka.


Mwanasheria Mkuu wa Jimbo la Lagos na Kamishna wa Haki, Lawal Pedro (SAN), alibainisha hayo siku ya jana Jumatatu Oktoba 21, katika mkutano na waandishi wa habari ambapo amesema ripoti imepokelewa.


Kulingana na Pedro, "Katika kesi ya Mohbad, ninakubali kumekuwa na kucheleweshwa na ucheleweshaji unachukuliwa kuwa nje ya muda uliopangwa kwa ajili ya uchunguzi.


"Uchambuzi wa kitaalamu toxicology, yote haya ni sehemu ya uchunguzi na nadhani tunachopaswa kujifunza ni kwamba kuhusu makosa ya jinai, hakuna hali ya ukomo kwenye uchunguzi.


“Kwa hiyo, ni bora kuwa na uchunguzi kamili wa ushahidi ambao unaweza kusababisha, angalau kutiwa hatiani kwa kesi inayowasilishwa mahakamani, kuliko kunyamaza kimya na kukimbilia mahakamani.


“Ni watu wale wale wanaolalamikia ucheleweshwaji ambao watakuwa ni watu walewale wa kusema mtu huyo alifikishwa mahakamani baada ya wiki moja, akaachiliwa na kuachiwa huru kwa sababu tu upelelezi haujakamilika.


“Kama uchunguzi haujakamilika ni vyema tuwe na subira. Lakini, naweza kukuambia, ripoti ya kutoka Marekani imepokelewa kwa muda mrefu sasa na pia tunayo nakala.


"Lakini ninaelewa kuwa wanafamilia wa Mohbad pia wameomba pia kufanya uchunguzi wao huru wa kisayansi.


“Hata hivyo, hii isituzuie kwa kuwa ripoti imetoka. Nina hakika kama ushauri wa kisheria haukutolewa wiki iliyopita, unapaswa kutoka wiki hii. Na wale watakaofunguliwa mashtaka watachukuliwa hatua kutokana na ushahidi uliopo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad