Sakata la Timu ya NIGERIA Libya, Kumbe ilikuwa ni Figisu ili Wachoke

Sakata la Timu ya NIGERIA Libya, Kumbe ilikuwa ni Figisu ili Wachoke


Timu ya taifa ya Nigeria iliamua kurejea nyumbani [Nigeria] bila kucheza mchezo wao wa kufuzu AFCON 2025 dhidi ya Libya baada ya kukutana na vitendo ambavyo walivitafsiri ni hujuma kutoka kwa wenyeji wao [Libya].


Inaelezwa kuwa, ndege maalumu iliyobeba wachezaji, benchi la ufundi, viongozi na watu wengine walioambatana na timu ya taifa ya Nigeria ilizuiwa kutua kwenye uwanja wa ndege wa Benina [mji ambao mechi ilipangwa kuchezwa] badala yake ilielekezwa ikatue kwenye mji wa Al Abaq [KM 230 kutoka Benina].


Sababu ya kuambiwa wakatue mji wa Al Abaq ni kujaa kwa uwanja wa ndege wa mji wa Benghazi. Kila walipoulizia kurusha ndege kutoka Al Abaq kwenda Benina waliambiwa bado uwanja wa ndege hauna nafasi hivyo wanapaswa kusubiri.


Inaelezwa watu wote waliokuwa kwenye ndege walikwama uwanja wa ndege wa Al Abaq kwa zaidi ya saa 13 bila kula chochote! Vilevile wachezaji wa Nigeria wanadai kwamba walikuwa wanasachiwa na maofisa wa Libya.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad