Shirika la Afya duniani WHO Yatangaza Nchi ya Kwanza Afrika Kutokuwa na Ugonjwa wa Malaria
Shirika la Afya duniani WHO, limeithibitisha rasmi Misri kuwa nchi isiyokuwa na Malaria jambo linaloashiria hatua muhimu sana katika vita dhidi ya ugonjwa huo.
Hatua hii ni kauli yenye kuonyesha nguvu ya juhudi za pamoja kati ya Serikali ya Misri, wafanyakazi wa sekta ya afya na ushirikiano wa kikanda.
Misri inakuwa nchi ya pili barani Afrika kufikia hatua hiyo ndani ya mwaka 2024, jambo linalothibitisha kuwa zana na mikakati ya sasa katika kudhibiti ugonjwa wa Malaria ni madhubuti.
Nchi zingine za barani Afrika ambazo zilishathibitishwa ni Cape Verde (2024), Algeria (2019) na Mauritius (1973).Mafanikio haya ni ya kutia moyo na hamasa kwa mataifa mengine.