Simba Hoi Kwa Coastal Union Ligi Kuu, Walazimishwa Sare ya Kibabe Sana

 

Simba Hoi Kwa Coastal Ligi Kuu, Walazimishwa Sare ya Kibabe Sana

Vigogo, Simba SC wamepunguzwa kasi baada ya kulazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Coastal Union ya Tanga leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge Jijini Dar es Salaam.


Simba waliuanza vizuri mchezo huo na kwenda mapumziko wakiwa wanaongoza 2-0 kwa mabao ya beki na Nahodha wake, Mohamed Hussein 'Tshabalala' dakika ya 25 na mshambuliaji wake mpya, Mcameroon Christian Leonel Ateba Mbida kwa penalti dakika ya 40.


Coastal Union walirejea na mipango mipya kipindi cha pili na kufanikiwa kusawazisha mabao hayo kupitia kwa winga wake Mkenya, Hassan Abdallah Hassan dakika ya 47 na beki wa kushoto, Mkongo Hernest Briyock Malonga dakika ya 71.


Kwa matokeo hayo, Simba SC inafikisha pointi 13 katika mchezo wa tano, wakati Coastal Union inatimiza pointi tano katika mchezo wa saba.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad