Singida Black Stars yaendelea kugawa dozi Ligi Kuu

Singida Black Stars


Timu ya Singida Black Stars imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa CCM Liti mjini Singida.


Mabao ya Singida Black Stars leo yamefungwa na viungo Muivory Coast, Josaphat Arthur Bada dakika ya 54 na mzawa, Ayoub Reuben Lyanga dakika ya 65.


Kwa ushindi huo, Singida Black Stars iliyo chini ya Mbelgiji, Patrick Aussems inafikisha pointi 22 katika mchezo wa nane na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tatu zaidi ya vigogo, Simba SC baada ya wote kucheza mechi nane.


Kwa upande wao Fountain Gate baada ya kipondo cha leo wanabaki na pointi zao 16 za mechi tisa sasa nafasi ya nne.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad