Taarifa za Wanachama wa CHADEMA Kuhamia CCM ni za Uongo

Taarifa za Wanachama wa CHADEMA Kuhamia CCM ni za Uongo

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Simiyu kimekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni zikidai kuwa Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Itilima amefunga ofisi za chama na kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM). Taarifa hizo zimetajwa kuwa si za kweli na zinapaswa kupuuzwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza, Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Simiyu, Mussa Onesmo, amesema kuwa Katibu Mkuu wa CCM, Emmanuel Nchimbi, alisikika akitoa taarifa hizo wakati wa ziara yake kijijini Luguru, Simiyu. Hata hivyo, Onesmo amesisitiza kuwa taarifa hizo ni za uongo kwani CHADEMA haina mwenyekiti wa Wilaya ya Itilima anayeitwa Telly Maduhu wala katibu anayeitwa Ngasa Mipawa, majina yaliyotajwa na CCM.

Kwa upande wake, Jackson Luyombya, ambaye ni Mwenyekiti halali wa CHADEMA Wilaya ya Itilima, amesema amesikitishwa na taarifa zilizotolewa kwenye mkutano huo, akieleza kuwa Mwenezi wa CCM alidanganywa ili kutoa mvuto kwenye ziara yake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad