Tamasha la WASAFI Festival Lasitishwa kwa Muda

 

Tamasha la WASAFI Festival Lasitishwa kwa Muda

Kamati ya Wasafi Festival 2024 imetangaza kusitisha kwa Muda Muendelezo wa Tamasha La Wasafi Festival 2024 ambalo lilikua linaendelea kwenye baadhi ya Mikoa Nchini kutokana na Msiba wa Khadija Shaibu (Dida) uliotokea Oktoba 4, 2024 ili kutumia muda huu kuomboleza na kuyaenzi Maisha ya Dida.


Taarifa ya KAMATI hiyo imesema “Khadija Shaibu (Dida) alikua ni mmoja kati ya Wadau wakubwa wa Burudani sio tu Redioni bali hata kwenye Matamasha mbalimbali makubwa ya Muziki na aliweza mara kadhaa kuandaa Matamasha yake ya Muziki wa Taarabu katika Maeneo Tofauti Tofauti nchini.”


“Hivyo Kuondoka kwake sio pigo tu kwa wasikilizaji na wapenzi wake, bali ni pigo pia kwa kamati nzima ya Tamasha la Wasafi Festival.”


“Kamati ya Wasafi Festival 2024, itatangaza tarehe ya Muendelezo wa Tamasha hili pale itakapokua tayari, Lakini katika kipindi hiki tungependa kuendelea kuyaenzi na kuyasheherekea Maisha ya MALKIA WA KIΡΑΖΑ Khadija Shaibu (Dida).”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad