TEN HAG MAMBO MAGUMU MAN UNITED, AOMBA USHAURI

TEN HAG MAMBO MAGUMU MAN UNITED, AOMBA USHAURI
Erik ten Hag

 

Kocha wa Manchester United, Erik ten Hag amesema anapenda kusikiliza wachambuzi kwani wapo wanaomsaidia kujenga timu wanapomkosoa.


Hivi karibuni, Ten Hag alimcharukia mchambuzi wa soka, nyota wa zamani wa Liverpool, Jamie Redknapp hana akili, baada ya kudai kuna kitu hakipo sawa baina yake na Marcus Rashford na wengine wakidai wana ugomvi na ndiyo maana hakumwanzisha kwenye mchezo uliopita wa Ligi Kuu England dhidi ya Crystal Palace na aliingia kuchukua nafasi ya Amad Diallo.


Hata hivyo, kocha huyo wa mashetani wekundu amesema anasikiliza zaidi kauli za wale wanaomkosoa kwani zinamsaidia awe imara na kuimarisha timu yake.


"Wengine wanatoa ushauri mzuri sana. Kwangu ushauri bora ni unaoeleza maeneo yenye upungufu, lakini huu ni mchezo wa soka unapoutumikia lazima ukubali kukosolewa."


"Sielewi wanavyokosoa. Watu wana haki ya kukosoa kama wanataka, lakini hawana haki ya kuleta tetesi ambazo si za kweli."


Amesema pia hatilii maanani kila uchambuzi kwani kila mtu anaongea anachokijua ingawa baadhi wanatoa maoni yanayomsaidia kujenga.


"Siwezi kutilia maanani kila lawama au ukosoaji, huwa sisomi kila kitu na muda mwingine sitakagi sana kujua kuhusu ukosoaji, jambo la msingi kwangu ni kufuata utaratibu wangu na kuiongoza timu kwenye njia sahihi na kuhakikisha nachukua hatua zinazofaa ili kupata matokeo bora."


Kocha huyo raia wa Uholanzi pia alisema wachezaji wake watarajie lawama nyingi kwa sababu kila mtu anataka washinde kila mechi.


"Watahukumiwa kwa kila mchezo na hiyo ni kawaida. Kila mtu anatarajia Man United kushinda kila mechi, ni kazi ambayo unaikubali unapokuwa unaingia kwenye timu hii na ndiyo jambo tunalolifanyia kazi kwa sasa, lazima tukabiliane na hili na kupata kilicho bora zaidi, ili kuendana na matarajio ambayo kila mtu anayo ingawa tunafahamu wachezaji ni wachanga, kikosi cha vijana, timu bado mpya, itachukua muda kufika tunapotaka," alisema Ten Hag na kuongeza,


Tunaenda katika uelekeo mzuri kwa sasa, katika wiki kadhaa zilizopita kwenye nyanja nyingi za soka, sasa tunaangalia namna ya kuwa na ufanisi kwenye mabao."

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad