TIMU ya JK Tanzania Yapata Ajali ya Basi



Basi la timu ya JKT Tanzania FC likiwa na wachezaji, benchi la ufundi na wafanyakazi wengine wa timu, likitokea Dodoma kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara dhidi ya Dodoma Jiji, limepata ajali na kusababisha maumivu kwa baadhi ya wachezaji na wafanyakazi wengine waliokuwemo kwenye basi hilo.

Basi hilo likiendeshwa na MT 92327 Cpl Hassani Bakari Darajani, limepata ajali 27 October 2024, saa 1:00 asubuhi eneo la Mbweni baada ya kuacha njia na kuanguka mtaroni.

Baadhi ya wachezaji waliopata maumivu na wako chini ya uangalizi wa madaktari ni Dany Lyanga, John Bocco, Salum Gado na Gamba Matiko.


Wengine ni Said Ndemla, Yakoub Suleiman, Hassan Dilunga, Maka Edward, Hassan Kapalata, Hassan Machezo na Mohamned Bakari.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad