TIMU YA YANGA PRINCESS YATINGA FAINALI NGAO YA JAMII, YAIFUNGA SIMBA

TIMU YA YANGA PRINCESS YATINGA FAINALI NGAO YA JAMII, YAIFUNGA SIMBA


Timu ya Yanga Princess imetinga fainali Ngao ya Jamii baada ya kuiondosha Simba Queens kwa mikwaju ya penalti baada ya mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Yanga imetinga fainali baada ya kushinda kwa mikwaju 4-3 dhidi ya Simba katika Uwanja wa KMC Complex jijini Dar es Salaam.

Yanga itakipiga fainali ya Ngao ya Jamii na JKT Tanzania Oktoba 5, mwaka huu katika uwanja wa KMC Complex.

JKT Queens ilitangulia fainali baada ya kuichakaza Ceasiaa Queens mabao 7-0 mapema leo.

Hii ni mara ya pili kwa Shirikisho la Soka nchini (TFF) kuleta michuano hiyo kwa wanawake tangu ilipochezwa msimu uliopita na Simba Queens ikichukua ubingwa kwa kuitoa JKT kwa mikwaju ya penati 5-4 dakika 90 zikitamatika kwa sare ya 1-1.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad