TMA imedai kuwa maeneo machache yanatarajiwa kupokea mvua nyingi kwanzia kesho. Kulingana na taarifa tulizozipata, mikoa ya ukanda wa ziwa Victoria na Magharibi inatarajiwa kupokea mvua nyingi na ngurumo za radi wikendi. Utabiri wa hali ya hewa nchini Tanzania kwa saa 24 zijazo: Mikoa ya Katavi, Kigoma, Kagera, Geita, Mwanza, Shinyangu, Mara na Simiyu hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo zinatarajiwa katika maeneo machache na vipindi vya jua wakati wa asubuhi hadi wakati wa mchana.
Vile vile visiwa vya Unguja na Pemba, mkoa ya Daresalaam na Tanga, Mikoa ya pwani, kulingana na habari tulizozipata mvua nyepesi wakati wa jioni na usiku zinatarajiwa. Pia vipindi vya jua vinatarajiwa wakati wa mchana. Wakazi wahimizwa kujiandaa ipasavyo.
Kanda ya ziwa Victoria, mikoa ya Kagera, Geita, Shinyangu, Mwanza, Shinyangu. Vipindi vya mvua vitavyoambatana na ngurumo za radi katika baadhi ya maeneo vinatarajiwa kwanzia kesho.
Nyanda za juu Kaskazini-mashariki, Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro inatarajiwa kupokea kupokea vipindi vya jua wakati wa asubuhi hadi wakati wa mchana. Mvua nyepesi nyepesi ngurumo za radi zinatarajiwa kuendelea maeneo mengi ya ukanda huu.