Try Again: Pesa sio SHIDA zetu Simba....

 

Try Again: Pesa sio SHIDA zetu Simba....

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugezi ya Simba, Salim Abdallah `Try Again’, amesema walivyojipanga msimu wa 2024/25 wanauwezo wa kumsajili mchezaji yoyote wanayemtaka ndani na nje ya Afrika kulingana na mapendekezo ya benchi la ufundi.


Kauli hiyo ni baada ya kuwepo kwa tetesi kuwa Simba wapo kwenye mchakato wa mazungumzo na kiungo wa Azam FC, Feisal Salum Fei Toto katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo lilalotarajiwa kufunguliwa Desemba.


Akizungumza na Spotileo, ‘Try Again’ amesema wanafanya usajili kulingana na mahitaji ya benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Fadlu Davids, akipendekeza usajili wa kiungo huyo, itafanyika hilo wani fedha sio tatizo.


Amesema kwa hawajafikiria suala la usajili kwa sababu bado hawajapokea mapendekezo kutoka benchi la ufundi, endapo akihitajika ya Fei Toto hawashindwi kumsajili kwa sababu wanauwezo wa kusajili mchezaji yoyote.


“Kama Kocha Fadlu anamtaka Fei Toto basi Simba haisiti kumsajili tunaenda kukutana na klabu yake kukaa meza moja kwa ajili ya mazungumzo ya biashara hakuna kinachoshindikana, sio yeye hata mchezaji yoyote yule. Hakuna mtu aliyetegemea tutamsajili Mpanzu kwa sababu usajili wa nyota huyo ulitusumbua na kumaliza soli ya viatu.


Tulipambana sana safari za DR Congo na mataifa mengine ya Ulaya kwenda kwa ajili ya kuonana na wanaomsimamia kwa ajili ya kupata saini yake, usajili wake ulitutesa sana lakini Mwekezaji na Rais wa heshima wa Simba, Mohammed Dewji alipambana na kutumia fedha kufanikiwa kumsajili,” amesema Try Again.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad