Tuchel Atamrithi Erik Ten Hag Manchester United?

 

Tuchel Atamrithi Erik Ten Hag Manchester United?


Uongozi wa Klabu ya Manchester united huenda ukamfuta kazi kocha wake raia wa Uholanzi Erik ten Hag, Baada ya mwenendo mbovu wa timu hiyo na nafasi yake huenda ikachukuliwa na kocha wa zamani wa Chelsea Thomas Tuchel, ambaye jina lake limepewa uzito na uongozi wa juu wa Klabu hiyo.


Viongozi wakuu wa klabu hiyo, akiwemo mmiliki mwenza Sir Jim Ratcliffe, wanatarajiwa kuwa na mkutano wa muda mrefu Jumanne, na nafasi ya kocha huyo Mholanzi huenda ikawa miongoni mwa mada muhimu zitakazojadiliwa katika kikao hicho.


Ten Hag amekuwa chini ya uchambuzi mkali katika wiki za hivi karibuni, na gazeti la Manchester Evening News limeripoti kwamba klabu ina mpango wa kumchukua Tuchel, mwenye umri wa miaka 51, baada ya michezo saba tu na kuanza vibaya katika kampeni mpya ya Ligi Kuu ya uingereza.


Wagombea wengine kwa nafasi hiyo wanapewa heshima na viongozi wa Manchester United, lakini Manchester evening news (MEN) inaripoti kwamba upatikanaji wa Tuchel unamfanya awe mgombea mkuu ikiwa Ten Hag atafutwa katika majukumu yake.


Mabingwa hao mara 20 wa ligi ya uingereza, walikuwa na hamu ya kumchukua Tuchel wakati wa kiangazi baada ya kuondoka kwake Bayern Munich, na viongozi wa klabu ya Manchester United walifanya mazungumzo na Mjerumani huyo kuhusu nafasi hiyo. Hata hivyo, United bado inaonekana kuzingatia mpango wa kumchukua Tuchel, na meneja huyo Mjerumani bado yupo wazi.


United imeshinda michezo miwili tu ya ligi hadi sasa, ikitoka sare miwili na kupoteza mitatu. Ikiwa na pointi nane tu, huu ni mwanzo mbaya zaidi wa ligi tangu msimu wa 1989-90 walipomaliza katika nafasi ya 13 chini ya Sir Alex Ferguson, Huku mechi yao ya mwisho ya ligi wametoka sare ya bila kufungana katika dimba la Villa Park hapo jana. ikiwa ni mchezo wao wa tano mfululizo bila ushindi.


Alipoulizwa kuhusu mustakabali wake baada ya mchezo huo, Ten Hag alisema; “hakuna mawasiliano kati yangu na viongozi wa United yaliyopendekeza kuondoka kwangu, Hivyo sina wazo lolote lililo tofauti,” aliongeza kuwa, “Wangeweza kunieleza tunawasiliana kwa uwazi sana, kwa uwazi kabisa.”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad