Ukata wa Fedha Barcelona, Kumpeleka Lamine Yamal EPL

 

Ukata wa Fedha Barcelona, Kumpeleka Lamine Yamal EPL

Mchezaji wa Barcelona Lamine Yamal amekuwa akihusishwa na uhamisho wa kuhamia kwa miamba wa Ligi ya Uingereza, Arsenal na Liverpool.


Vyanzo vinaripoti kuwa Barcelona wanaweza kufikiria kumuuza kinda huyo mwenye miguu ya dhahabu aliye na umri wa miaka 17 kutokana na matatizo ya kifedha yanayoikabili klabu hiyo.


Katika siku za karibuni Barcelona imekuwa ikiandamwa na madeni mazito, na kwa sababu hiyo manguli kwenye biashara ya soka wanaamini kuwa haitakuwa jambo la kushangaza kama Barca itaamua kumuweka kinda huyo sokoni .


Pamoja ya kwamba Arsenal na Liverpool vimetajwa kuwa vilabu vinavyoitamani sana saini ya mchezaji huyo, lakini ieleweke kuwa hakuna uhamisho wala biashara yoyote itakayoweza kufanyika hadi Julai 2025 wakati winga huyo atakapofikisha umri wa miaka 18.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad