Vifo vya Watoto Mapacha Tegeta Kamanda wa Polisi Afunguka


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema linafanya uchunguzi wa vifo vya kutatanisha vya watoto mapacha ambao walifariki baada ya kunyweshwa uji na mama yao katika eneo la Tegeta.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam , Jumanne Muliro amesema uchunguzi huo unafanywa kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali, ikiwemo Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (CGCLA) na pindi uchunguzi utakapokamilika, maelezo zaidi kuhusu chanzo cha vifo yatatolewa kwa umma.

Taarifa ya vifo vya watoto hao ilisambazwa kupitia mitandao ya kijamii Oktoba 5, 2024, ikimuonesha mama wa mapacha waliofariki, Mwajuma Amani, akisimulia jinsi watoto wake walivyoonekana kuwa na afya nzuri hadi walipokunywa uji na kisha hali yao ikabadilika.

“Nilikuwa nimewapa uji vizuri, lakini nikawakuta wanashindwa kupumua, wakapoteza fahamu. Niko katika hali ya kuchanganyikiwa na sijui hasa kilichowapata mapacha wangu,”Aliskika akisema mama huyo amesikika akisema mama huyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad