Wadau Wasanaa Wamtetea Steve Nyerere Kuendelea Kutumia Jina la Nyerere



Wadau wa Sanaa na mashabiki wa filamu na vichekesho wamemtetea Msanii Steve Mengele kuhusiana na kuendelea kutumia jina la Nyerere.

Hapo jana, Msemaji wa Familia ya Hayati Mwalimu Nyerere alisema kuwa wasanii wanaotumia jina la Nyerere akiwemo Steve waache mara moja kwani wanaleta mkanganyiko kwa familia kwa wengine kudhani kuwa watu hao ni wanafamilia ya Nyerere.

Kupitia mitandao ya kijamii, wadau mbalimbali wameonesha kupinga kauli hiyo kwa kusema kuwa msanii huyo alipewa jina hilo na mashabiki wake baada ya kuwa anaigiza sauti ya Hayati Mwalimu Nyerere kwa ufasaha na kwamba Nyerere ni jina la mtu kama yalivyo majina mengine kwa hiyo hawaoni shida msanii huyo kulitumia.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad