Yanga SC imepangwa Kundi A Ligi ya Mabingwa Afrika katika droo iliyofanyika leo mjini Cairo, Misri. Timu nyingine katika kundi hilo ni TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), El Hillal ya Sudan na MC Alger ya Algeria.
Wajue wapinzani wa Yanga Sc ( Mc Alger ) MC Alger kirefu chake ni Mouloudia Club d’Alger ambapo ilianzishwa mwaka 1921 nchini Algeria ni moja kati ya Club zenye historia kubwa Algeria ila kuanzia 1977 hadi 1986 ilikuwa ikijulikana kama Mouloudia Pétroliers d’Alger.
MC Alger sio timu ya kubeza hata kidogo sio kwa sababu viwango vya soka la Afrika Kaskazini vipo juu au Algeria ipo juu katika viwango vya FIFA lakini ndio Club ya kwanza ya Algeria kuwahi kushinda CAF Champions League mwaka 1976.
Ni moja kati ya vilabu vyenye mafanikio Algeria wamewahi kushinda Ligi Kuu ya Algeria mara 7 na mwaka 1976 ndio ilikuwa mara yao ya kwanza kufuzu kucheza Club Bingwa Afrika baada ya kushinda Ligi Kuu Algeria na ilifanikiwa kufika hadi fainali ya michuano hiyo na kuifunga Hafia Conakry ya Guinea.
MC Alger ni Club inayotumia uwanja wanao tumia ni Ramadhan Stadium au Stade Omar Hamadi uliyopo katika mji mkuu wa Algeria (Algers) timu hiyo hutumia jezi zenye rangi Nyekundu,nyeupe na kijani.
Kwa sasa MC Alger ipo nafasi ya tano wakicheza Michezo mitatu katika msimamo wa Ligi Kuu Algeria unaoshirikisha timu 16, MC Alger iliyo nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi imecheza mechi 3 imeshinda mechi moja kufungwa mechi 0 na kutoka 2 mechi 3.
RATIBA: CAF CHAMPIONS LEAGUE
26/27-11-24: Yanga vs Al Hilal
06/7-12-24: MC Alger vs Yanga
13/14-12-24: Mazembe vs Yanga
03/4-01-25: Yanga vs Mazembe
10/11-01-25: Al Hilal vs Yanga
17/01-01-25: Yanga vs MC Alger.