Wafanyakazi Wanne Taasisi ya Mikopo ya OYA Wanaotuhumiwa Kuua Wamefikishwa Mahakani

Wafanyakazi Wanne Taasisi ya Mikopo ya OYA Wanaotuhumiwa Kuua Wamefikishwa Mahakani

Wafanyakazi Wanne Taasisi ya Mikopo ya OYA Wanaotuhumiwa Kuua Wamefikishwa Mahakani


Wafanyakazi wanne wa taasisi ya mikopo ya OYA wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kibaha kwa tuhuma za mauaji ya kukusudia ya Juma Said Seif (45), mkaazi wa Kitongoji cha Mbagala Mlandizi Mkoani Pwani yaliyofanyika Oktoba 7. 2024.

Wakili wa Serikali, Monica Mwela amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Dastan John Charles (23), Christopher John Charles (23), Emmanuel Joshua Olala(24) ambao ni wakazi wa Kilangalanga Mlandizi pamoja na Abdallah Felix Wendiliwe (32) mkaazi wa Janga Mlandizi.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kibaha, Emmaeli Lukumai amesema ushahidi wa kesi hiyo iliyosomwa kwa mara ya kwanza bado haujakamilika, hivyo kesi hiyo imehairishwa hadi Oktoba 30 mkwaka huu.

Wakati wakisomewa kesi hiyo, watuhumiwa hawakutakiwa kujibu lolote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya mauaji. Watuhumiwa wote wamerudishwa rumande.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad