Wakazi: Tuzo za MZIKI zisitumike Kisiasa, BASATA Wala Wizara Wasihusike...

Wakazi: Tuzo za MZIKI zisitumike Kisiasa, BASATA Wala Wizara Wasihusike...



Siasa za kwenye Tuzo ni tatizo sugu na lina pande tatu; MASSAGING EGOS, BALANCING EMOTIONS & MANAGING EXPECTACTIONS.

Nilihudhuria Tuzo 2022, kila mtu badala ya kushukuru team yake, producers, writers, management, anasema, “Tunamshukuru Rais”.
Tuzo zikitumika as “propaganda machine”, anayeumia ni MUZIKI. Tanzania ina potential kimuziki, ila tumenasa sababu hatuchukui hatua stahiki; na Tuzo kutumika kisiasa haisaidii.

Wasanii wenye MAUDHUI ya KISIASA na UANAHARAKATI kutopata nafasi. I mean by Umaarufu, Streaming Numbers na Impact, wimbo wa Roma wa “NIPENI MAUA YANGU” unapaswa kuwa nominated! Kwa Standards za kibongo, wimbo hauna neno na ulikuwa lead song iliyo propel auze vizuri album yake.
Sasa tunawalindaje kina Roma, Nay Wa Mitego, Wakazi, Vitali Maembe,nk, kupata fair-share ya Tuzo bila kujali mitazamo na itikadi.
Kumbuka Nyuma ya Tuzo kuna BASATA, ambao recently wamekuwa kama Polisi wa Sanaa na sio Walezi.

Pia Tuzo zikiwapa ushindi Artists ili WASINUNE, je tutakuwa tunaitendea haki Tasnia? Nimeona Zuchu kaongelea hilo. Yaani it looked obvious kuwa kuna BALANCING inafanyika, kwenye category na kwenye ushindi

Why GOSPEL MUSIC wamenyimwa Category? Wao wanataka, ila nyie kwa sababu za KISIASA hamtaki kisa Waislamu hawataki KASWIDA na nyie mnaona kama moja ikiwepo na lazima nyingine iwepo. Sasa mbona Category nyingi tu hamjaziweka? Infact kwenye Hip Hop hamna Male & Female?

SUGGESTION: Serikali iweke structure kwa Tuzo kufanyika, ila isiwe ina interfere kitu and let the music play!
Kuwe na Uhuru wa kuwepo Tuzo mbali mbali, na BASATA wala WIZARA isihusike.

Academy izingatie MUZIKI na sio WASANII. Focus iwe kwenye muziki bora na uliofanya vizuri. Tusiangalie Majina wala ku-balance ili wote wafurahi. YOU CANT PLEASE EVERYBODY! Kama kuna wimbo unastahili kushinda kila kitu acha ushinde. Imagine Mwaka ambao Darassa alitoa “Muziki”, tungeshangaa yeye kushinda kila kitu?

Kuwe na Category ya BEST INSPIRATIONAL MUSIC ambapo Gospel na other inspirational music will fall under. Muziki wa Kiislamu ni Ibada, ila isiwe sababu ya Gospel kushindwa kupewa maua yao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad