Waliokufa Kwa Ajali ya Boti Nchini Congo Wafika 80


WALIOKUFA MAJI CONGO AJALI YA BOTI WAFIKA 80

Waokoaji katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wanaendelea kuwatafuta watu walio hai au waliokufa maji baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kupinduka na kuzama
katika Ziwa Kivu, mashariki mwa Jamhuri hiyo.

Hadi sasa taarifa kutoka DRC zinaeleza kuwa watu takribani 80 wamethibitika kufa maji katika ajali hiyo.

Idadi kamili ya watu waliokuwamo ndani wakati boti hiyo inazama haijafahamika, hivyo imekuwa ni vigumu kufahamu idadi kamili ya waliokufa maji na wale waliookolewa wakiwa hai.

Mara kwa mara maafisa wa sekta ya uchukuzi wa DRC wamekuwa wakionya tabia ya baadhi ya wamiliki wa vyombo vya majini kupakia abiria na mizigo kupita uwezo wa vyombo husika, hali ambayo imekuwa ikisababisha ajali za mara kwa mara.

Mwezi Juni mwaka huu boti iliyokuwa imejaza mizigo kupita uwezo wake ilizama karibu na mji mkuu wa DRC, Kinshasa na kusababisha vifo vya watu 80.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad