Yanga Haijashuka, Kitakwimu Inaonyesha Wameimarika Zaidi Msimu Huu




Binafsi sijaona mahala Yanga imeshuka katika eneo lolote ukilinganisha na msimu uliopita kwa idadi ya magoli waliyofunga na idadi ya mechi

Ni vile kuna aspects 2 zinaleta mkanganyiko

Overexpectations on New signings

Below standards showcase of overexcited signings

Ila overall analysis Yanga haijashuka standards eneo lolote

Kimataifa msimu uliopita Yanga Sc mechi 4 za mwanzo walifunga jumla goli 11 wakiruhusu bao 1

Katika ligi mechi 7 za mwanzo walifunga jumla goli 20 wakiruhusu matano

Msimu huu kimataifa Yanga wamefunga jumla ya bao 16 wakiruhusu bao 1

Katika ligi Yanga wamefunga jumla ya bao 13 mpaka sasa bila kuruhusu bao

Kwenye mechi kushinda Jumla Kimataifa (4) na Ligi (7)

Msimu uliopita Yanga walishapoteza mchezo mmoja katika mechi 11 na kuruhusu mabao 6 michezo yote.

Msimu huu Yanga hajapoteza mchezo hata mmoja akiwa karuhusu bao 1 pekee michuano yote.

Wapi kwa takwimu hizi Amedrop?

Hoja ya Walisajiliwa kutoonyesha makali inaeleweka ila Yanga wameendelea kutumia sources zao za mabao na zinalipa huku wakiwa wameimarika eneo la ulinzi zaidi .

Kumbuka baadhi ya sajili mpya pamoja na kuimarika kwa ushindani msimu huu zimelazimu Gamondi afanye mabadiliko ya kimbinu hata aina ya uchezaji kwa sasa imebadilika ila Overall Analysis haionyeshi mahala Yanga ana madhaifu hayo katika mijadala.

Ila kuhusu kushuka kiwango Sio kweli kuhusu Kushuka

Matazamio ni Akina Baleke na Dube kutokuwa katika wafungaji na usajili mpya

Ila ukiitazama timu imeimarika kuliko msimu uliopita.

Maana Hajaruhusu bao
Ana additional Chama ambaye sasa safu ya Ushambuliaji wana Pacome, Chama, Aziz Ki na Maxi huu utajiri kuna timu wanayo?

Ila pia tusibeze tutazame Ushindani wa ligi kukua na kuleta chachu ya big games nyingi zenye mvuto na ushindani kabla ya kutafuta kasoro za Yanga Sc ambazo kitaalamu Sio kweli.

Itazame Top 5 ya ligi tazama numbers za Singida na FG fc tazama soka la ushindani.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad