Yanga na Azam Kupigwa Chamazi Complex, Wenye Uwanja Wakataa

 

Yanga na Azam Kupigwa Chamazi Complex, Wenye Uwanja Wakataa

MCHEZO wa Dar es Salaam Derby kati ya Yanga dhidi ya Azam FC, utakaopigwa Jumamosi, Novemba 2, uwanja wa Azam Complex, uliopo Chamazi badala ya Benjamini Mkapa, jijini.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu, Almas Kasongo amesema wengi walitamani mechi ichezwe uwanja wa Benjamini Mkapa, waliwaandikia barua wamiliki wa uwanja huo, bahati mbaya kutokana na uwanja huo uko kwa maboresho.

“Maombi yao hayakuweza kukubaliwa lakini unaweza kuelewa kwamba uwanja upo katika matengenezo makubwa na mkandarasi anahitaji muda zaidi na amepewa tarehe ya mwisho wa kukamilisha hiyo kazi kwa hiyo.

Imeonekana itakuwa changamoto ya kuweza kumsimamisha kutoendelea na hilo jambo kuwaruhusu Yanga. Kwa hiyo wamekataliwa tafsiri yake ni kwamba muda wa kikanuni kuwa wanaweza wakaenda nje, uwanja wao wa nyumbani unaweza usipate zile siku 21,” amesema Kasongo.

Amesema kwa hali hiyo kwa mujibu wa kanuni Yanga wanatakiwa kucheza uwanja wake wa nyumba ambao (Azam Complex), bodi kushirikiana na Yanga, wamiliki wa uwanja wako katika mazungumzo ya jinsi ya viingilio ili kuweza kuangalia takwimu za mashabiki watakaoingia kulingana na idadi ya uwanja.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad