Yanga waendeleza Ubabe Ligi Kuu, waichapa JKT Tz Chamazi

Yanga waendeleza Ubabe Ligi Kuu, waichapa JKT Tz Chamazi

 Yanga waendeleza Ubabe Ligi Kuu, waichapa JKT Tz Chamazi

Mabingwa watetezi, Yanga SC wameendeleza rekodi ya ushindi wa mechi zote tangu kuanza kwa msimu wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya Jana Jumanne kuichapa JKT Tanzania mabao 2-0 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.


Mabao ya Yanga katika mchezo huo yamefungwa na viungo wanyumbulifu, Muivory Coast Peodoh Pacôme Zouzoua dakika ya 23 na Mzambia, Clatous Chita Chama dakika ya 44.


JKT Tanzania ilimaliza pungufu baada ya kipa wake, Dennis Richard kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 39 kufuatia kudakia nje ya eneo lake shuti la Pacome.


Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 18 katika mchezo wa sita na kurejea nafasi ya pili, nyuma ya Singida Black Stars yenye pointi 19 za mechi saba. Kwa upande wao, JKT Tanzania baada ya kichapo cha leo inabaki na pointi zake 10 za mechi nane sasa nafasi ya saba

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad