Chalamila Atoa Tamko Kali Kwa Wanaokusanya Michango Bila Utaratibu Kupitia Ajali Ghorofa la Karikoo



Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amewaonya baadhi ya Watu wanaotumia janga la kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo kutapeli kwa kuchanganisha michango kinyume na taratibu kuacha mara moja akisema wanaweza kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Akiongea RC Chalamila amesema “Nitoe rai kwamba tumekwishaanza kupata minong’ono ya baadhi ya Watu kuanza kutumia tukio hili kinyume na utaratibu na sheria zilizopo za maafa kwa wote ambao wanatumia mwanya kutapeli Watu kuwa na ‘lipa namba’ ambazo hazijthibitishwa ama kuwa na ‘lipa namba’ ambazo wanatumia jina la Serikali kujinufaisha naomba nitoe rai kwamba wanaweza kuchukuliwa hatua kali za kisheria”

“Muda huu sio wa kujinufaisha bali ni wa kuwaokoa wenzetu, sisi kama Serikali na Mhe. Rais amekwisha elekeza kwamba gharama zote za msingi zibebwe na Serikali na Ofisi ya Mhe. Waziri Mkuu ndio itakayoratibu masuala yote ya gharama kuanzia majeneza hadi usafiri”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad