Comoro ni nchi yenye jumla ya watu 872,836. Nchi ambayo biashara kuu ni kilimo na Uvuvi
Nchi isiyo na ligi imara, wala wachezaji wanaocheza nje, IMEWASHANGAZA WENGI na imeandika record kushiriki AFCON kwa mara ya kwanza tangu kuumbwa kwa dunia.
Oktoba 23, 2024. Comoro ilimteua kocha Stefano Cusin kuwa kocha wao mkuu. Huyu mwamba aliwahi kuwa kocha msaidizi wa Wolves Fc ya England kipindi ipo Championship…
Stefano Cusin alifanya Comoro iwe timu ngumu kufungika. Chini ya uongozi wake Comoro imeshinda mechi 12 na kufungwa mechi moja tu.
Comoro inaenda AFCON kwa mara ya kwanza huku ikiwa na record bora. Katika mechi 6 za Group lao ambalo walikuwepo Tunisia, Gambia na Madagascar. Comoro wao wameshinda mechi tatu, sare tatu huku wakikusanya jumla ya points 12
Comoro wameongoza kundi lao kwa points 12, huku wakitoa dozi takatifu kwa Tunisia na Gambia yenye mastaa kibao kutoka Ulaya
Sababu hizi zinatosha kabisa kukuonyesha ni namna gani Comoro haijafika hapo kwa kubahatisha. Walijipanga na kwa umoja wao wamefanya mabalaa
Comoro ni kati ya team chache ambazo zimefuzu AFCON bila kufungwa mechi yoyote, na bila kupoteza mchezo wowote kwenye uwanja wa nyumbani
Lakini pia Inawezekana AFCON ya mwaka 2025 ikawa na utamu wake kutokana na timu ambazo hazikutegemewa kutoboa kibabe.
Timu kama Botswana, Sudan na Comoro ambazo hapo mwanzo zilionekana ni timu za kinyonge zisizo na mbele wa nyuma zimeingia AFCON kwa kishindo.