Democrats Wajutia BIDEN Kugombea Urais Mwanzoni

Democrats Wajutia BIDEN Kugombea Urais Mwanzoni


Spika wa zamani wa Baraza la Wawakilishi la Marekani, Nancy Pelosi, amesema chama cha Democrat kingeweza kufanya vyema katika uchaguzi wa Jumanne kama Rais Joe Biden angejiondoa mapema kwenye kinyang'anyiro hicho.


Pelosi, ambaye ni mmoja wa wanasiasa wenye ushawishi mkubwa Washington, amesema kwenye mahojiano na gazeti la New York Times kwamba Biden angejiondoa mapema, kungekuwa na nafasi pana kwa wagombea wengine kuingia kwenye kinyang’anyiro.


Kauli hii ya Pelosi imeibua mjadala mkubwa ndani ya chama cha Democrat, ambao wameshindwa kufanikiwa kupata Ikulu ya White House huku pia kukiwa na uwezekano wa kupoteza udhibiti wa mabunge yote mawili.


Pelosi amekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha mabadiliko ya uongozi ndani ya chama, ambapo inaripotiwa aliongoza shinikizo la kumtaka Biden aachie nafasi hiyo. Hatimaye, Biden alijiondoa mwishoni mwa Julai, lakini ni baada ya wiki kadhaa za kushinikizwa kufuatia matokeo yasiyoridhisha katika mdahalo dhidi ya Donald Trump.


Baada ya kujiondoa, Biden alimuidhinisha haraka Makamu wa Rais Kamala Harris kuwania nafasi hiyo, lakini siku ya Jumanne, alishindwa vibaya na Rais mteule Donald Trump. Pelosi ameendelea kueleza kuwa hatua ya Biden kumwidhinisha Harris haraka ilizuia nafasi ya kuwa na uchaguzi wa mchujo ulio wazi. Anasema kuwa, kama kungekuwa na muda wa kutosha kwa mchakato wa mchujo, Harris angefanya vyema na kuwa na nguvu zaidi.


"Lakini kwa sasa, tunaishi na kile kilichotokea,” amesema Pelosi, akisisitiza kuwa hatua hiyo ingeweza kutoa nafasi bora zaidi kwa wagombea wenye ushindani mkubwa kutoka ndani ya chama.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad