Rais Mteule wa Marekani #DonaldTrump amewateua Elon Musk na Mgombea Urais wa zamani wa chama cha Republican, Vivek Ramaswamy, kuongoza Idara ya Ufanisi wa Serikali.
Trump alisema kwenye taarifa kwamba Musk na Ramaswamy "watafungua njia kwa utawala wangu kuvunja urasimu serikalini, kupunguza kanuni zisizo za lazima, kupunguza matumizi ya kupindukia, na kurekebisha mashirika ya serikali ya shirikisho."
Kwa muda mrefu Elon Musk alikuwa ameomba kuanzishwa kwa idara ya ufanisi wa serikali na amekuwa akiipigia debe bila kuchoka. Trump alisema shirika hilo litafanya ukaguzi kamili wa kifedha na utendaji kwa serikali nzima ya shirikisho na kutoa mapendekezo ya mageuzi makubwa.