Nadhani Gamondi alijisahau. Raha zilimzidi kuliko kujali changamoto ambazo zilikuwa zinamkabili mbele yake. Huwa inatokea kwa wachezaji na makocha wengi ambao wanatua nchini na kufanya vizuri. Hakuna nchi tamu kuishi kama Tanzania. Maisha ni matamu. Maisha yana raha. Mashabiki nao wanaiangalia siku ya leo tu ambayo wametoka kushinda mechi."
"Pale Zanzibar saa moja tu baada ya Yanga kuwafunga CBE, Gamondi aliungana na sisi kupata kinywaji. Hakuonekana kuijali tena mechi. Maisha yake yamejaa raha kwa sasa."
Anasema Edo kumwembe