Emmanuel Nchimbi : Awatetea Wagombea Waliokatwa, Atoa Ombi Kwa Waziri Mchengerwa

Emmanuel Nchimbi : Awatetea Wagombea Waliokatwa, Atoa Ombi Kwa Waziri Mchengerwa


Katibu Mkuu wa CCM, Emmanuel Nchimbi kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ametoa wito kwa Wizara ya TAMISEMI kupuuza makosa madogomadogo katika hatua ya mwisho ya kusikiliza rufaa za mapingamizi ili kuwapa Watanzania wengi zaidi nafasi ya kugombea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili kutoa hamasa ya demokrasia kuendelea kukua Nchini.

Akiongea leo November 12,2024, Jijini Dar es salaam, Nchimbi amesema “Natoa wito wa CCM kwa Waziri mwenye zamana na Serikali za Mitaa, kwamba tunatambua wamefuata sheria lakini ni muhimu kukumbuka kwamba demokrasia yetu bado ni changa inahitaji kukua, tutachukua muda kujifunza makosa yataendelea kupungua, tunaiomba TAMISEMI katika hatua ya mwisho ya rufaa kuyapuuza makosa madogomadogo ili Watanzania wengi zaidi wapate nafasi ya kugombea”

“Msimamo wa CCM ni huu na nasisitiza msimamo huu ninaoutoa una baraka za Mwenyekiti wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan”

Kauli ya Nchimbi inakuja kufuatia malalamiko ya Vyama vya Upinzani ikiwemo CHADEMA na ACT kulalamikia majina ya Wagombea wao kuenguliwa kwasababu mbalimbali ambapo baadaye Waziri wa TAMISEMI Mohamedi Mchengerwa aliagiza wenye malalamiko kupeleka mapingamizi ambapo tayari mapingamizi yamewasilishwa kwa Mamlaka na sasa hatua inayoendelea ni usikilizwaji wa rufaa za Wagombea walioenguliwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad