Freeman Mbowe Afunguka: Hatujitoi Uchaguzi Serikali za Mitaa

Freeman Mbowe Afunguka:  Hatujitoi Uchaguzi Serikali za Mitaa


 Freeman Mbowe Afunguka:  Hatujitoi Uchaguzi Serikali za Mitaa

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe amesema Chama hicho hakitojiondoa kwenye ushiriki wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa licha ya changamoto wanazoendelea kukutana nazo za kuenguliwa kwa majina yao.


“CHADEMA imejengwa kwa maumivu makubwa sana , CCM inalipwa kodi zetu na inajaribu kupambana na upinzani wakati wao wana fedha, wanajigamba wamepita kwa asilimia 100 wakati Dunia nzima inaona wakiengua Watu wetu, wengi wanalia wanasema Mwenyekiti tujitoe kwenye Uchaguzi huu wengine wanasema tupambane mpaka damu ya mwisho, Kamati Kuu yetu iliyokaa Mtwara tulikubaliana pamoja na mapungufu yote tushiriki uchaguzi”


“Kwenye maeneo walikoenguliwa washauriane katika ngazi zao wajue wachukue hatua gani, Viongozi w- CHADEMA msikae tu kusubiri Mbowe aseme, chukueni hatua msisubiri agizo kutoka juu”


“Mwaka 2019 tulijitoa kwenye uchaguzi baada ya majina kuenguliwa sana lakini mwaka huu hatujitoi, Wanaharakati mbalimbali walienda Mahakamani kuzuia TAMISEMI kusimamia uchaguzi waliyaona haya, laiti Mahakama zetu zingechukua hatua haya yasingetokea lakini Mahakama zetu zina Watu wa ajabu CCM inalindwa hata ikitenda dhambi za wazi, tunaiomba Mahakama ya rufani ipige zuio” ———— Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akiongea na Waandishi wa Habari Makao Makuu ya CHADEMA leo November 19,2024 Mikocheni Jijini Dar es salaam

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad