Dk 45 za kwanza Namungo walionekana kung’ata meno - Wakifika kwenye kila tukio kwa wakati kwenye yale maeneo ambayo Yanga walikua wanapitisha mipira yao.
Coach Mgunda aliamua kuwaheshimu Yanga na kuwaachia wacheze mpira wao. Setup ya Namungo 4-4-2 katika wakati wa kukaba iliwanyima nafasi Yanga kutumia nguvu yao kati kati. Option pekee ilibaki kupitia pembeni ambako Yanga walikua hawana makali sana.
Pembeni Yanga hawakua na ufanisi. Kwanini?
Yao Kouassi na Kibabage ambao walikua wakitegemewa kumwaga maji ndani, hawakua na usahihi wa krosi. Kibabage mara kadhaa ameonekana kukosa ufanisi wa krosi zake ambazo mara nyingi zinakua hazina nguvu wala kuwa na macho ya kufika kwenye boksi kwa usahihi. Hii iliwanyima Yanga uwezo wa kuwa na options za kutengeneza mashambulizi yao
Ni dk 45 za kwanza ambazo Yanga alitengeneza clear-chance moja pekee ambayo Aziz Ki alishindwa kufunga bao kwa mzungusho wake uliokula mwamba.
Yanga ilirudi vipi kipindi cha pili?
Kwanza, Max alirudishwa kucheza zaidi kama winga ya kushoto tofauti na mwanzo alipokua anapokelea mpira zaidi kwenye left half space. Hii iliwapa Yanga advantage ya kutanua defence line ya Namungo na kupata nafasi za kupitisha mipira kutoka kwa mido zao.
Ni nyakati hii ambayo Yanga imefanya ‘tactical-switch’ ndipo Max alipata nafasi ya kutoa nafasi ya bao kwa Musonda.
Namungo walishindwa kuendana na kasi ya ‘Ujanja Ujanja’ wa Ramovic kubadilisha mfumo kipindi cha pili. Hii ilimpa Mgunda wakati mgumu asijue nini cha kufanya. Na hata alipoamua kuitoa timu chini ianze kushambulia, still Yanga walikua bora kuyameza mashambulizi yote ya Namungo ambayo yalikosa UTU na UTULIVU.
Duke Abuya - Hii ni mali. Nimependa perfomance yake ya leo. Utulivu wa upigaji pasi, nidhamu ya kucheza kwenye eneo lake. Wakati Yanga wanajiuliza nani atavaa viatu vya Aucho, Abuya akawajibu kwa vitendo; Nipeni viatu vya Aucho, nifunge kamba, nichape pasi za upendo, mpate pira burudani.
Ushindi wa kwanza kwa Ramovic ligi kuu, ushindi wa muhimu kwa Yanga kurudisha morali yao.
FULL TIME: Namungo 0-2 YANGA
𝐅𝐔𝐋𝐋 𝐓𝐈𝐌𝐄 : NBC Premier League
NAMUNGO FC 0-2 YOUNG AFRICANS SC
⚽️ 46” Musonda
⚽️ 67” Pacome