Hizi Ndio Sababu Kadhaa Ziara ya Rais Samia Nchini Cuba Kuhairishwa

Rais Samia


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, amesema ziara ya Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan imeahirishwa kufuatia taarida ya kuchafuka kwa hali ya hewa kutokana na Kimbunga Rafael kulikosababisha viwanja vya ndege kufungwa Cuba kwa zaidi ya saa 48.

Akiongea leo November 07,2024, Waziri Kombo amesema “Wizara inapenda kuwaatarifu Umma na Wananchi wote Tanzania kwamba ziara ya Rais Samia iliyopangwa kufanyika hapa Havana Cuba kati ya November 6 hadi November 8,2024 imeahirishwa rasmi hivi sasa kutokana na taarifa ya awali ya kuchafuka kwa hali ya hewa na dhoruba inayoitwa Rafael kupiga katika visiwa vya Cuba na Mji wa Havana na kupelekea viwanja vya ndege vyote vya Cuba kufungwa kwa saa zaidi ya 48”

“Hivi sasa Kimbunga kimeshapita na shughuli zimeanza kurudi katika hali yake ya kawaida kwa muktadha huo safari ya Rais Nchini Cuba itafanyika siku usoni ambapo itatolewa taarifa maalum ya kufanyika safari hiyo”

“Kwa upande wa tamasha na kongamano la Kimataifa la lugha ya Kiswahili Duniani Mh. Rais ameagiza ziendelee kama kawaida na zitaongozwa na Mawaziri tulio hapa nikiwemo Mimi na Waziri Ndumbaro na Waziri wa Afya Mhagama “

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad