Huyu Hapa Mrithi wa Kocha Gamondi Yanga

 

Huyu Hapa Mrithi wa Kocha Gamondi Yanga

Uongozi wa klabu ya Yanga umemtaka Kocha wake, Miguel Gamondi ajieleze kwa nini usimfute kazi kutokana na matokeo ya kupoteza mechi mbili mfululizo za Ligi kuu ya NBC na kutoelewana na wasaidizi wake .

Kamati tendaji ya klabu hiyo imempa siku moja kujieleza kwa nini isimfute kazi.

Leo Jumapili November 10, Uongozi wa Klabu hiyo unatarajiwa kuamua hatma ya Miguel Gamondi kubaki au kuondoka.

Taarifa ambazo ni za ndani zinadai kuwa kwa asilimia kubwa Gamondi anaondoka Yanga na kocha Kheireddine Madoui ndiye mrithi wake.

Gamondi anatajwa kuondoshwa Yanga kutokana na vitu vingi lakini mwenendo mbaya wa timu hiyo kwenye mechi 2 za mwisho umetajwa kuwa sehemu tu.

Jeuri, kiburi, kutoshaurika, ubishi, kupoteza ushawishi kwenye timu na wachezaji (dressing room) kutoelewana na wasaidizi wake vinatajwa kuwa vitu vinavyomuondoa Gamondi Yanga.

Inasemekana mpaka sasa Gamondi anaelewana na msaidizi wake mmoja tu ambaye ni Moussa Ndaw.

Taarifa zaidi zinasema kuwa Ndaw huenda naye akaondoka na bosi wake Gamondi ili kupisha utawala mpya.

Kuna habari za Gamondi na kocha wa makipa kurushiana maneno makali katika hoja ya kutoelewana na wasaidizi wake.

Kheireddine Madoui ambaye anatajwa kuirithi mikoba ya Gamondi ni raia wa Algeria mwenye umri wa miaka 47 ni kocha wa CS Constantine ambao wapo Kundi moja na Simba SC CAF Confederation Cup 2024/2025.

Klabu hiyo ipo nafasi ya 1 kwenye Msimamo wa Ligi Kuu ya Algeria (Algerian Ligue 1) ikiwa inacheza mechi 8, ikikusanya pointi 15.

Kheireddine Madoui amewahi kuchukua CAF Super Cup 2015, Algeria Ligue 1 2014/2015 na 2016/17, Algeria Super cup 201 5 na 2017.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad