Katibu wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) Wilayani Kilolo Mkoani Iringa aitwae Christina Kibiki, usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake eneo la Kijiji cha Ugwachanya, Kata ya Mseke, Tarafa ya Mlolo ameuawa kwa kupigwa risasi na Watu ambao bado hadi sasa hawajajulikana.
Mmoja wa Watoto wake amesema kwamba Watu hao ambao walikuwa watatu walifanya uvamizi huo usiku wa jana saa tatu nyumbani kwa Marehemu na kumuulizia kama yupo ambapo walipoambiwa yupo ndani wakamfuata hadi chumbani na kumuua.
“Majira ya saa 3 usiku mlango uligongwa na Mtu mmoja na kumuulizia Mama kama yupo wakamuambia ndio na Bibi akatoka ili kuangalia ni nani ambaye anamuulizia, baadae wakaongezeka Watu wawili na kisha mmoja akamsukuma Bibi na kuingia nae chumbani ndipo na sisi tulisikia ‘paaa” (mlio wa risasi) tukaanza kupiga kelele na wao wakatoka wakakimbia“
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Allan Bukumbi amesema Marehemu alifariki wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Tosamaganga kutokana na kupigwa risasi eneo la kifuani pamoja na kitu kizito kichwani “Jeshi la Polisi linachukunguza tukio hilo”