Kauli ya Kwanza ya Kamala Harris Baada ya Kushindwa Uchaguzi Marekani

Kauli ya Kwanza ya Kamala Harris Baada ya Kushindwa Uchaguzi Marekani


Makamu wa Rais wa Marekani na Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Democratic, Kamala Harris, ametoa hotuba ya kukubali kushindwa uchaguzi wa Rais uliofanyika siku ya Jumanne na Donald Trump kuibuka Mshindi ambapo amempongeza Trump wa Republican kwa kuchaguliwa tena kuliongoza Taifa hilo.


Akiwahutubia maelfu ya Wafuasi wake mbele ya majengo ya Chuo Kikuu cha Howard Mjini Washington, Harris amewataka Wafuasi wake kutokata tamaa, akiwataka waendelee kupigania masuala yaliyochochea shauku yao wakati wa kampeni “Mapambano ya uhuru wetu yanahitaji kazi ngumu lakini kama navyosema siku zote tunapenda kazi ngumu, kazi ngumu ni kazi nzuri, mapambano kwa ajili ya Nchi yetu yana thamani”


“Kwa Vijana mnaotazama ni sawa kuhuzunika na kujisikia vibaya lakini tambueni kila kitu kitakuwa sawa, kwenye kampeni nilisema tukipambana tutashinda lakini wakati mwingine mapambano huchukua muda hii haimaanishi hatutoshinda, kitu muhimu ni kwamba usikate tamaa , usikate tamaa kamwe, usiache kujaribu kuifanya Dunia kuwa eneo zuri, una nguvu na kamwe usimsikilize Mtu yoyote anayekuambia kitu hakiwezekani kwakuwa hakijawahi kufanywa kabla”


Harris ambaye kabla ya hotuba yake alimpigia simu Trump kukubali kushindwa na kumpongeza, amesema yeye na Rais Joe Biden watasaidia kufanikisha mabadilishano ya madaraka kwa njia ya amani.


Katika hatua nyingine, Rais Biden pia ameongea na Rais Mteule Trump kwa njia ya simu ambapo amempongeza kwa ushindi aloupata kwenye uchaguzi wa November 5 na kumkaribisha kuitembelea Ikulu ya White House wakati akijiandaa kuchukua hatamu za uongozi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad