Kijana Ferdnand Ndikuriyo (27) maarufu kwa jina la Chuma Cha Chuma ambaye ni Raia wa Burundi, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam leo November 05,2024 akikabiliwa na mashitaka ya kuishi Nchini Tanzania bila kibali.
Chuma ambaye ni Mkazi wa Mbezi Louis, Dar es salaam, amefikishwa Mahakamani hapo na kusomewa mashitaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ushindi Swalo ambapo Wakili wa Serikali kutoka Uhamiaji, Ezekiel Kibona, amedai Chuma alitenda kosa hilo September 18,2024 eneo la Upanga, Las Vegas Casino Wilaya ya Ilala Dar es Salaam na kwamba akiwa eneo hilo alibainika kuwepo Nchini bila kibali.
Baada ya kusomewa mashitaka yake Mshitakiwa huyo amekana kutenda kosa hilo huku Wakili wake akidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika hivyo kuiomba Mahakama iwapangine tarehe nyingine ya kutajwa.
Mahakama hiyo inatarajia kutoa uamuzi kesho November 6, 2024 juu ya hatma ya kumpa dhamana ama lah ambapo Mshtakiwa huyo amepelekwa Mahabusu