Serikali ya Equatorial Guinea imesema hivi karibuni itafunga camera maalum za ulinzi kwenye Ofisi zote za Serikali ili kudhibiti vitendo viovu vya uvunjifu wa maadili vinavyofanywa kwenye Ofisi hizo ikiwa ni uamuzi ambao umekuja kufuatia kashfa ya ngono inayomuhusisha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kitaifa la Uchunguzi wa Fedha Nchini humo, Baltasar Engonga ambaye amejirekodi akifanya mapenzi na Wanawake zaidi ya 400 Ofisini kwake na nyumbani.
Makamu wa Rais wa Equatorial Guinea, Teodoro Obiang Nguema Mangue amesema hayo baada ya kufanya kikao na Viongozi wa Mamlaka za Serikali kujadili kashfa ya video hizo za ngono ambapo amesisitiza hawatovumilia vitendo vinavyochafua taswira ya Uongozi na Serikali ya Nchi hiyo
Ebang ambaye ni Baba wa Familia ya Watoto sita, tayari amekamatwa kwa kosa la kujirekodi akiwa anafanya mapenzi na Wanawake hao ambao wengine ni Wake za Watu akiweno Mke wa Kaka yake, Binamu yake, Dada wa Rais wa Nchi hiyo, Mke wa Mkuu wa Ulinzi wa Rais wa Nchi hiyo, Mke wa Mwanasheria Mkuu wa Nchi hiyo na Mtoto wa Mkuu wa Jeshi la Polisi la Nchi hiyo.
Wengine walioonekana wakifanya mapenzi na Ebang kwenye video hizo ni Mke wa Mlinzi wake (Bodyguard), Mke wa Mchungaji wake, Wake wa Mawaziri kadhaa wa Nchi hiyo, Mke wa Mjomba wake ambaye ni Mjamzito, Marafiki 15 wa Mdogo wake wa kike na Wanawake wengine mbalimbali ambapo imeelezwa wote hao walionekana kuridhia video hizo kurekodiwa