Kocha Aliyefukuzwa Timu ya Taifa ya Ghana, Aipeleka Timu ya Sudan AFCON....

Kocha Aliyefukuzwa Timu ya Taifa ya Ghana, Aipeleka Timu ya Sudan AFCON....


Mwaka 2019 - Rais wa Shirikisho la Soka Ghana alimfukuza Kazi Kwesi Appiah na rasmi hakua tena kocha wa Ghana. Sababu ya kufukuzwa ilikua kutumia ‘Wachezaji wasiojulikana’. Moja ya mchezaji huyo asiejulikana kwa wakati huo alikua ni huyu Mohamed Kudus

20 Sept 2023 - Sudan ilimteua Kwesi Appiah kuwa kocha wao mkuu, kwa ahadi ya kumpatia mshahara wa Dola 50,000 kwa mwezi.

Kwesi Appiah, alianza kukisuka taratibu kikosi cha Sudan kwa ajili ya mechi za ushindani. Huku zaidi ya 95% ya wachezaji wake wanatokea Sudan ndani ndani huko, na baadhi wakitokea kikosi cha Al Hilal na El Merreikh

Kuelekea AFCON 2025 Qualifiers, Sudan alipangwa kundi moja na Ghana, Niger & Angola.

Kwesi akajiapiza, kwa kuwa Ghana ( Timu yake ya taifa) imepangwa kundi moja na timu anayofundisha ambayo ni Sudan, basi lazima awatembezee kichapo. Appiah alikua na hasira ya kufukuzwa kipindi kile akiwa kocha wa Ghana

Mungu si Athumani! Sudan alimchapa Ghana na kutoa sare nae katika mechi 2 za kufuzu kwenye group lao. Sudan aliondoka na points 4 mbele ya ‘Big-Fish’ Ghana, huku Kwesi Appiah akienda kuchekea chooni

Sudan imemaliza kundi ikiwa nafasi ya pili na points 08, huku Ghana ya Kwesi Appiah ikimaliza wa mwisho kwenye kundi ikiwa na points 03 pekee.

Kwa mbaaaali Ghana wanamtamani sana Kwesi, ila yeye mwenyewe anasema — NO WAY, SUDAN NI TIMU YA NDOTO ZANGU

We call it, SWEET REVENGE

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad