Kocha Aliyempiga REFA Ngumi Afungwa Jela Miaka Mitatu

Kocha Aliyempiga REFA Ngumi Afungwa Jela Miaka Mitatu


Mahakama Nchini Uturuki imemuhukumu kifungo cha miaka mitatu na nusu Rais wa zamani wa Club ya soka ya MKE Ankaragucu aitwae Faruk Koca, kwa kosa la kumshambulia Refa Halil Umut Meler baada ya mchezo wa ligi kuu ya Super Lig dhidi ya Caykur Rizespor msimu uliopita.


Tukio hilo lilitokea baada ya mechi kumalizika kwa sare ya 1-1 ambapo Mashabiki walivamia uwanja mara tu baada ya Rizespor kufunga bao la kusawazisha dakika za mwisho mnamo tarehe 11 Desemba 2023.


Pamoja na Koca, Watu wengine watatu walioshiriki katika shambulio hilo la kumdhuru Mwamuzi walihukumiwa vifungo vya Gerezani kati ya mwaka mmoja hadi mitano ambapo Koca alijiuzulu nafasi yake kama Rais wa Klabu hiyo muda mfupi tu baada ya tukio hilo na inaelezwa kuwa anatarajiwa kukata rufaa dhidi ya mashtaka hayo, hapo awali alikamatwa na kuwekwa rumande kwa muda kabla ya kuachiwa kwa dhamana.


Kutokana na tukio hilo, klabu ya Ankaragucu ilipigwa faini ya lira milioni 2 za Uturuki sawa na (milioni 150 TZS) na iliamuriwa kucheza mechi tano za nyumbani bila Mashabiki huku Refa huyo akilazwa Hospitalini kwa ajili ya matibabu baada ya kupata jeraha dogo karibu na jicho lake

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad