Kocha Miguel Angel Gamondi hafurahishwi kabisa kuutumia uwanja wa azam complex nakusema ndio unasababisha Yanga kupata matokeo mabaya.
Taarifa za ndani zinadai Yanga ipo katika mchakato wa kutafuta uwanja Mpya wa Nyumbani baada ya kuona Uwanja wa Azam unachangia wao kupoteza mechi.
Kocha Gamondi amesema hakipendi kiwanja hicho kwasababu ni kidogo hakiwapi nafasi wachezaji wake kuonesha ufundi haswa wapinzani wanapoamua kukaa nyuma.
Aidha baadhi ya watu wameona ni rahisi kufanyiwa hujuma kwenye uwanja huo wa Azam kwasababu wenye uwanja pia wanalitaka kombe.