Kocha Moallin wa KMC Atambulishwa Yanga, Kodro Kumsaidia Ramovic



Kocha Moallin wa KMC Atambulishwa Yanga, Kodro Kumsaidia Ramovic


Abdihalim Moalin rasmi ametambulishwa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Yanga huku wakitarajia kushusha mwingine mpya.

Klabu ya Yanga imemtambulisha rasmi aliyekuwa kocha wa KMC Abdihalim Moalin kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa timu hiyo, huku msaidizi wa Ramovic akitua.

Moalin ambaye ni kocha wa zamani wa Azam aliachana na KMC hivi karibuni na muda mchache uliopita ametangazwa kuchukua cheo hicho kwenye kikosi cha Yanga nafasi ambayo ni mpya.

Mtu wa mwisho kushika nafasi hiyo ndani ya Yanga alikuwa kocha Mholanzi Hans van Der Pluijm wakati timu hiyo kocha mkuu akiwa Mzambia, George Lwandamina kipindi cha uongozi wa Bilionea marehemu Yusuf Manji.

Yanga pia imemrudisha Hafidh Saleh ambaye alikuwa nje ya kikosi hicho baada ya awali kuondolewa wakati wa utawala Gamondi.

Mara baada ya kuondolewa kwa Gamondi, Mwananchi limepata taarifa ya kurudishwa kwa Hafidh ambaye ataendelea na cheo chake cha Mratibu wa Klabu hiyo. Mwanachama huyo alikuwa ndani ya benchi la ufundi na uongozi kwa vipindi mbalimbali.

"Mabadiliko haya yanalenga kuongeza ufanisi na sio kwamba kuna shida kubwa sana, wapo ambao wana shida lakini wapo wengine wameamua wenyewe kuondoka na Kamati ya Utendaji ikabariki," alisema mmoja wa mabosi wa timu hiyo.

Msaidizi ni huyu

Klabu ya Yanga imemtambulisha rasmi Mustapha Kodro kuwa kocha msaidizi akichukua nafasi ya Moussa N'Daw raia wa Senegal.

Kodro anaenda kuongeza nguvu katika benchi jipya chini ya kocha mkuu, Sead Ramovic wakiwa na jukumu la kuiongoza timu hiyo katika michezo ijayo kwa kuanza na hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika Novemba 26 mwaka huu.

Kondro ambaye alikuwa msaidizi wa Ramovic pale TS Galaxy, amezaliwa Agosti 29, 1981, huko Mostar nchini Bosnia-Herzegovina huku akiwa na leseni ya UEFA Pro.

Kabla ya kuwa kocha, Kodro katika kipindi chake cha kucheza soka alikuwa kiungo mkabaji, akizitumikia Zvijezda na FK Velez Mostar zote za Bosnia-Herzegovina.

Ikumbukwe kwamba, Ramovic alipokabidhiwa mikoba ya kuifundisha Yanga amewabakisha makocha wengine wote waliokuwa wasaidizi kwa Gamondi akiwemo kocha wa viungo Taibi Lagrouni, kocha wa makipa Alaa Meskini na mchambuzi wa mikanda ya video Mpho Maruping.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad