Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa.
Kwa mujibu wa ripoti iliyoundwa na aliyekuwa Waziri Mkuu na kujiuzulu Edward Lowassa, kati ya ghorofa 505 ambazo zilikaguliwa, 147 zilikutwa hazina nyaraka za ujenzi.
Lowassa aliunda tume baada ya jengo la hoteli ya Chang’ombe Village Inn. Iliyokuwepo Keko kuanguka mwaka 2006 na kuua mtu mmoja na kujeruhi wengine kadhaa.
Madai ya awali ni kwamba kulikuwa na ukiukwaji katika ujenzi wake. Jambo ambalo lilimsukuma Edward Lowassa, kuunda tume haraka sana ya kukagua ghorofa zote za Dar.
Waziri Mkuu wa baada yake Mizengo Pinda aliliambia Bunge kuwa tume hiyo ya Lowassa, ilibaini kuwa ukaguzi huo, pia ghorofa 81 zilikiuka masharti ya ujenzi.
Huku ghorofa zingine 22 wahusika wenye nazo hawakupatikana na zilijengwa bila kuzingatia taratibu na sheria za ujenzi.
"Can you imagine, mtu anaamua kupandisha ghorofa lake hapo bila kufuata taratibu za mamlaka husika, hii ni hatari kubwa," alisema Pinda wakati akitoa majumuisho ya hotuba ya matumizi ya ofisi yake bungeni kwa mwaka 2008/09.
Pinda alisema ghorofa nyingi zinazojengwa Dar es Salaam, zinajengwa holela bila kufuata taratibu za ujenzi.
Lowassa aliunda tume, na kuagiza majengo yote yasiyofuata utaratibu. Na yale yaliyo katika hatari ya kubomoka kutokana na ujenzi wa ovyo, basi yabomolewe yote.
Mungu awapiganie wote walioathirika na janga hili.