KUMEKUCHA: Rais Ruto Asitisha Mkataba wa Adani Group Kuchukua Uwanja wa Ndege JKIA


KUMEKUCHA: Rais Ruto Asitisha Mkataba wa Adani Group Kuchukua Uwanja wa Ndege JKIA

Rais William Ruto ameagiza kusitishwa kwa Mkataba kati ya Serikali na Kampuni Adani Enterprises uliokuwa unalenga kuendesha na kuboresha miundombinu ya Sekta ya Anga na Nishati

Ruto ametoa agizo hilo wakati akihutubia Bunge leo Novemba 21, 2024 na kueleza kuwa uamuzi huo ni baada ya kuwepo ushahidi wa Vitendo vya Rushwa uliotolewa na mashirika ya uchunguzi dhidi ya Kampuni ya Adani

Uamuzi wa Serikali unakuja ikiwa ni saa kadhaa tangu Waendesha Mashtaka wa Marekani kumshtaki Mmiliki wa Adani Group, Gautam Adani kwa kusaidia utoaji Rushwa ya zaidi ya Tsh. Bilioni 663.45, kwa Maafisa wa Serikali ya India ili apate Tenda ya kusambaza Nishati ya Umeme wa Jua

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad