Kumekucha Uchaguzi Marekani, Donald Vs Kamala Harris Hapatoshi

 

Kumekucha Uchaguzi Marekani, Donald Vs Kamala Harris Hapatoshi

Baada ya muda mrefu wa kampeni na mivutano ya hapa na pale, Taifa la Marekani Leo hii Novemba 5 limeingia katika uchaguzi mkuu kitaifa, kumchagua Rais atakayeliongoza taifa hilo Kwa miaka minne ijayo.

Kwa mujibu wa Statista watu zaidi ya milioni 161.42 wamejisajili kupiga kura nchini Marekani, huku takwimu zikionyesha idadi kubwa ya vijana wamejiandikisha kupiga kura na kukiwa na ongezeko la watu wazima wenye umri wa miaka 35 mpaka 49, waliojitokeza ikiwa ni idadi kubwa kulinganisha na mwaka 2020.

Wagombea Urais Kamala Harris ( Democratic) na Donald Trump (Republican), wamechuana vikali katika kura za maoni ambapo kulingana na mtambo wa ufuatiliaji wa Kura za Kitaifa wa FiveThirtyEight, Harris anaongoza kwa asilimia 1, Trump ana asilimia 46.8 za dhidi ya asilimia 48.1 za Kamala Harris.

Hata hivyo, uongozi huo unapungua, ikionyesha kwamba kila mgombea ana nafasi nzuri ya kushinda kiti hicho.

Zoezi la kumtangaza Rais mteule wa Taifa hilo, linategemea jinsi zoezi la uchaguzi litakavyokamilika katika majimbo yote, mfano katika mwaka 2012 Rais Obama alitangazwa kabla ya saa sita usiku siku ya uchaguzi.

Siku ya Kuapishwa hutokea kila baada ya miaka minne tarehe 20 Januari au tarehe 21 Januari ikiwa tarehe 20 Januari itaangukia Jumapili. Sherehe ya kuapishwa hufanyika katika jengo la Capitol la Marekani huko Washington, DC. Huku Kwa awamu hii Sherehe ya kuapishwa kwa Rais ajaye imepangwa kufanyika tarehe 20 Januari, 2025.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad