Kwanini Diamond Platnumz Hajatajwa Tuzo za Grammy 2025

Kwanini Diamond Platnumz Hajatajwa Tuzo za Grammy 2025


Diamond Platnumz amekosa kutajwa kwenye Grammy 2025, jambo lililozua maswali kuhusu vigezo vinavyohitajika.

Muziki wa Diamond umejikita zaidi Afrika Mashariki na si kwa kiwango kikubwa kwenye masoko makubwa kama Marekani au Ulaya.

Grammy huzingatia ubora wa kiufundi na uandishi wa nyimbo, ambapo wasanii wanatakiwa kutoa ujumbe kwa ufasaha na ubunifu wa kipekee. Diamond ana vipaji, lakini ili kufikia kiwango cha Grammy, inahitaji ubora unaokubalika kimataifa.

Muziki unahitaji pia kuwa na ushawishi wa kimataifa, na kwa @diamondplatnumz, ingawa ana umaarufu mkubwa Afrika Mashariki, ni wachache wanaothamini muziki wake nje ya Afrika.

Msanii kama Burna Boy, ambaye ni mshindi wa tuzo ya Grammy, anatambuliwa kwa albamu zilizothibitishwa (certfied) kwenye masoko makubwa ya Marekani na Ulaya. Diamond hajafikia kiwango hicho kwa sasa.

Mbinu za masoko za kimataifa pia ni muhimu. Hatujasikia kampeni kubwa zinazomlenga msikilizaji wa soko la kimataifa, jambo linaloathiri umaarufu wake nje ya Afrika.

Licha ya mafanikio ya Bongo Fleva, muziki wa Tanzania unakutana na changamoto za utambulisho ikiwa ni pamoja na kushindana na muziki wa Nigeria na Afrika Kusini, ambao umekubalika zaidi kimataifa.

Kutokuwepo kwa Diamond kwenye Grammy 2025 si sababu ya kulaumu waandaaji wa tuzo, bali ni mwito kwa msanii na uongozi wake kuongeza juhudi kwenye masoko na kolabo za kimataifa, jambo litakalomsaidia sio tu Diamond, bali pia wasanii wengine wa Tanzania wanaoziota tuzo hizo za Kimataifa.

✍️: @enkyfrank

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad