Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelezea kupokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Lawrence Nyasebwa Mafuru, kilichotokea jana November 09, 2024 Hospitali Nchini India.
“Ninatoa pole kwa Familia, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), Prof. Kitila Alexander Mkumbo, Watumishi wa Tume ya Mipango, Ndugu, Jamaa na Marafiki kufuatia msiba huu”
“Mafuru atakumbukwa kwa utumishi wake uliotukuka, bidii na ubunifu alipotumikia nafasi mbalimbali ndani ya Serikali, Mwenyezi Mungu aijalie familia yake subra na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu na ailaze roho yake mahali pema, Amina” —- Rais Samia