Mambo Matano Yanayoivuruga Klabu ya Yanga kwa Sasa.

Mambo Matano Yanayoivuruga Klabu ya Yanga kwa Sasa.


Mambo yameendelea kuwa magumu klabu ya Yanga baada ya kukumbwa na misukosuko mingi ndani ya muda mfupi. Leo tarehe 15 Novemba Yanga wametangaza kuachana na waliokuwa makocha wa klabu hiyo ambao ni Miguel Gamondi kocha mkuu na Mousa Ndauw kocha msaidizi. Hizi ni nyakati mbaya kwa klabu hiyo na kuna uwezekano likawa anguko la klabu hiyo katika mbio za kutetea ubingwa wa ligi ya NBC na kombe la CRDB.

Nimekuandalia mambo matano yanayoivuruga klabu ya Yanga kwa sasa.

1.Kufungwa na Azam pamoja na Tabora United

Klabu ya Yanga ilianza vyema msimu wa 2024/25 kwa kushinda mechi 8 za awali na kuwa kinara kwenye msimamo wa ligi wakijikusanyia alama 24 na katika mechi hizo walifunga mabao 14.Mchezo dhidi ya Azam walipoteza kwa bao 1-0 na mchezo dhidi ya Tabora United walipoteza kwa mabao 3-1.Kupoteza michezo hiyo kuliibua gumzo klabuni hapo na hoja ya kumfukuza kocha Gamondi ilianza kuchochewa moto na hatimaye leo ametimuliwa.

Kama umetazama michezo hii miwili ambayo Yanga wamepoteza utagundua mwalimu hakuwa na tatizo lolote la kiufundi kwa sababu mchezo wa kwanza alimpoteza beki wake tegemezi Ibrahim Bacca aliyepewa kadi nyekundu lakini Yanga waliutawala mchezo huo,na mchezo dhidi ya Tabora alipata wakati mgumu baada ya mabeki tegemezi kama Dickson Job,Boka ,Yao Kwasi na Ibrahim Bacca ikamlazimu mwalimu kuwaanzisha Denis Nkane,Aziz Andambwile,Mwamnyeto na kwenye safu ya ulinzi . Hatujawahi kushuhudia kombo hii ikicheza pamoja na hata katika mchezo huo walikosa maelewano na kukatika mara kwa mara.


2. Kuondoka uwanja wa Chamazi Complex

Mara baada ya kupoteza michezo hiyo klabu ya Yanga ilitangaza kuuhama uwanja wa Chamazi unaomilikiwa na AzamFC na kuhamia uwanja wa KMC COMPLEX. Kuhama huko kulihusishwa na vitendo viovu kwa baadha ya mashabiki waliopoanza kurusha chupa za maji uwanjanji Taarifa kutoka bodi ya ligi imekiri kupokea barua ya maombi kutoka Yanga na imesema itashughulikia ombi hilo hivyo mpaka sasa Yanga hawana uwanja rasmi wa kucheza mechi zake za ligi kuu.


3. Kufungiwa Usajili

Barua rasmi kutoka FIFA imewaamuru TFF kuizuia klabu ya Yanga kufanya usajili wowote wa wachezaji wazawa na wakigeni baada ya kushindwa kumlipa Augustine Okrah ada yake ya usajili. Ukiachana na madai ya wachezaji Klabu hiyo imekumbwa na faini mbalimbali kwa hivi karibuni na zote chanzo ni utovu wa nidhamu kwa kutofuata kanuni na taratibu za TFF.

Klabu hiyo itaendelea na sajili za dirisha dogo mara baada ya kukamilisha malipo ya wachezaji wanaowadai.


4. Yanga Princess yafungwa na watani ligi ya wanawake

Klabu ya Yanga Princess imeendelea kufanya vibaya msimu huu baada ya kucheza michezo 4 ikipata sare 3 na kufungwa mchezo mmoja dhidi ya watani zao Simba Queens.Mwendelezo huu mbaya kwa Yanga Princess unaifanya klabu hiyo kushika nafasi ya 7 kati ya timu 10 zinazoshiriki ligi hiyo.

Mwenendo huo mbovu umeanza kuzua migogoro ndani ya klabu hiyo na kumfanya kocha wake mkuu Edna Lema kukalia kuti kavu. Klabu ya Yanga inapitia changamoto


5.Kumtimua kocha Gamondi na Mousa Ndauw


Gamondi na Ndauw kuondoka si jambo sahihi kwa uongozi wa Yanga.Makocha hao waliikuta ikitetea ubingwa wake msimu wa 2022/23 na waliiongoza klabu hiyo kutwaa makombe matatu ikiwemo kombe la Azam,Kombe la NBC ngao ya jamii pamoja na kufika fainali ya kombe la shirikisho Africa.

Gamondi aliisaidia Yanga kutwaa mataji mawili kwa msimu wa 2023/24 na kufika hatua ya robo fainali kwa mara ya kwanza kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Africa. Jambo la kukumbukwa kwa kocha huyo ni kuwafunga Simba mabao 5-1 msimu huo na mwanzoni mwa msimu wa 2024/25 Kocha huyo aliiongoza Yanga kutwaa kombe la ngao ya jamii.

Gamondi hakupaswa kuondoka Yanga kwani uongozi na mashabiki walikuwa wanamhitaji sana kutokana na umahili aliouonyesha siku za hivi karibuni


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad