Mapya yameibuka katika sakata la video 400 baada ya ripoti kudai kuwa Mke wa Mkurugenzi Mkuu aliyefutwa kazi wa Shirika la Kitaifa la Uchunguzi wa Fedha la Equatorial Guinea, Anie Baltasar Ebang Engonga, amenaswa katika mahusiano ya nje ya ndoa baada ya video moja ya ngono yenye sura yake kusambaa mtandao wa X.
Video hii yenye sura ya Mke wa Baltasar imesambaa kwenye mitandao ya kijamii Afrika huku wanaume wakiitumia kama njia ya kumkingia kifua Balthazar kwa kusema kuwa ‘sio tu mume tu aliyesaliti ndoa ata Mke wake ni msaliti pia.
Hatua hiyo imepelekea wadau kudhani kuwa huenda wawili hao walikuwa kwenye ndoa wazi (open marriage) kuwa kila mtu anaweza kuwa na mahusiano nje ya ndoa.