DEMOKRASIA: Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe kupitia akaunti yake ya mtandao wa X amelaani mauaji na kujeruhiwa kwa Wagombea, Viongozi na Wanachama wa CHADEMA akiwemo Steven Chalamila wa Jimbo la Tunduma, Modestus Timbisimilwa wa Kata ya Gongolamboto na George Juma Mohamed wa Kata ya Mkwese
Aidha, ametoa wito kwa Jeshi la polisi kuwaachia huru Wanachama na Viongozi wa chama hicho waliokuwa wakizuia kura batili na bandia kuingizwa katika vituo vya kupigia kura leo Novemba 27, 2024 wakati zoezi la upigaji kura likiendelea maeneo mbalimbali nchini